Kuja kwa Kristo kutakuwa kama ambavyo ingelikuwa usiku wa manane, wakati watu wote wakiwa wamelala. Itakuwa vema kwa wote kuandaa hesabu zao kikamilifu kabla ya jua kutua. Matendo yote yapaswa kuwa sahihi, biashara zote zapaswa kuwa za haki, kati ya mtu na mwenzake. Hali zote za kutokuwa waaminifu, mazoea yote ya dhambi yapaswa kutupiliwa mbali. Mafuta ya neema yapaswa kuwa katika vyombo vyetu pamoja na taa zetu. . . Kwa hakika itakuwa huzuni kwa yule ambaye hali ya roho yake imekuwa na mfano tu wa utauwa huku akizikataa nguvu zake; ambaye amekuwa akimuita Kristo Bwana, Bwana, na bado hana mfano wake wala maandiko yake. ..
Kwa neema Mungu
anatoa siku ya rehema, muda kwa ajili ya jaribio na maonjo. Anatoa
mwaliko: “Mtafuteni Bwana maadam anapatikana, mwiteni maana yu karibu”. .
.
Leo sauti ya rehema inaita, na Yesu anavuta watu kwa kamba za
upendo; lakini siku yaja ambapo Yesu atavaa mavazi ya kisasi. . . Uovu
wa dunia linaongezeka kila siku, na hatua fulani inapokuwa imefikiwa,
kitabu kitakuwa kimefungwa, na hesabu zitakuwa zimekamilishwa.
Hakutakuwa na kafara kwa ajili ya dhambi tena. Bwana anakuja. Kwa muda
mrefu rehema imenyoosha mkono wa upendo, subira na uvumilivu, kuelekea
kwa dunia yenye hatia. Mwaliko umetolewa, “Hebu na ashikilie nguvu
zangu...” Lakini watu wametumia vibaya rehema na kukataa neema.
Kwa nini Bwana amekawiza ujio wake hivyo? Jeshi zima la mbinguni linasubiri kukamilisha kazi ya mwisho kwa dunia hii iliyopotea, Kazi hiyo haijakamilishwa kwa sababu wachache wanaodai kuwa na mafuta ya neema katika vyombo vyao na taa zao, hawajakuwa nuru ing’aayo na kuiangaza dunia. Ni kwa sababu wamishenari ni wachache. . .
Kwa nini Bwana amekawiza ujio wake hivyo? Jeshi zima la mbinguni linasubiri kukamilisha kazi ya mwisho kwa dunia hii iliyopotea, Kazi hiyo haijakamilishwa kwa sababu wachache wanaodai kuwa na mafuta ya neema katika vyombo vyao na taa zao, hawajakuwa nuru ing’aayo na kuiangaza dunia. Ni kwa sababu wamishenari ni wachache. . .
Kila
juma linapopita linamaanisha juma moja limepungua, kila siku ipitayo
inaashiria siku moja ya karibu zaidi kufikia wakati uliowekwa kwa ajili
ya hukumu. Inasikitisha kwamba wengi wanayo dini ya msimu - dini
inayotegemea hisia na kutawaliwa na misisimko. “Yeye atakayevumilia hadi
mwisho ndiye atakayeokoka.” Hivyo jichunguzeni na kuhakikisha kama
mnayo mafuta ya neema ndani ya mioyo yenu. Kuwa na mafuta haya
kutatengeneza ule utofauti utakaohitajika katika hukumu.