NIWZEJE KUMPOKEA NA KUTOKA KATIKA MAUTI
1.Kiri mambo matatu
A.Mimi ni mwenye dhambi."Wote wametenda dhambi " RUM 3:23
B.Niko hatarini kufa."Mshahara wa dhambi no mauti"Rum 6:23
C.Siwezi kujiokoa ."Pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote"Yn 15:5
2.Baada ya toba hiyo amini mambo matatu
A.Alikufa kwa ajili Yangu."Aionje mauti kwa ajili ya kila MTU" Ebr 2:9
B.Amenisamehe.
C..Ameniokoa.
YATAFAKARI MAMBO HAYA KWA MUDA
#kwa sababu ya dhambi zangu nimehukumiwa kifo.
#siwezi kulipa fidia hiyo bila kupoteza uzima wa milele .
#ninadaiwa deni nisiloweza kulilipa.
#ni lazima niipokee zawadi hii.
Friday, 11 December 2015
Friday, 4 December 2015
UMUHIMU WA NENO LA MUNGU
UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU
Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa
maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema
mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya
uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima
| ||
Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16). Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni… A) Neno la Mungu li Hai B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6). C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11). b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11). c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6). Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12). Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo. Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11). Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35). Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3). |
Thursday, 3 December 2015
MUNGU HANA UPENDELEO
Warumi 9:14-33
Mungu Hana Upendeleo
14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?
22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa? 23 Na tunajuaje kama Mungu alifanya hivi ili kuwadhihirishia utajiri wa utukufu wake wale anaowahurumia, ambao aliwaandaa tangu mwanzo kupokea utu kufu? 24 Na sisi ndio hao walioitwa, si kutoka kwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.
Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko
25 Hivi ndivyo Mungu asemavyo katika kitabu cha Hosea, “Wale ambao hawakuwa watu wangu, nitawaita ‘watu wangu,’ na wale ambao hawakuwa wapendwa wangu, nitawaita ‘wapendwa wangu’.” 26 Na pale pale walipoambiwa,“Ninyi si ‘watu wangu,’ ndipo watakapoitwa, ‘Wana wa Mungu aliye hai’.” 27 Na Isaya anasema hivi kuhusu Israeli: “Ijapokuwa wana wa Israeli watakuwa wengi kama mchanga wa bahari, ni wachache tu miongoni mwao watakaooko lewa;28 kwa maana Mungu ataitekeleza hukumu yakejuu ya ulimwengu mara moja na kuikamilisha.” 29 Na tena kama alivyotabiri Isaya,“Kama Bwana wa majeshi asingetuachia uzao, tungalikuwa kama Sodoma, na kufanywa kama Gomora.”
30 Kwa hiyo tusemeje basi? Watu wa mataifa ambao hawakuta futa kupata haki wamepewa haki kwa njia ya imani. 31 Lakini Waisraeli ambao wametafuta kupata haki kwa msingi wa sheria, hawakuipata kwa maana hawakutimiza sheria. 32 Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani bali kwa kutegemea matendo. Wali jikwaa kwenye lile ‘jiwe la kujikwaa.’ 33 Kama ilivyoandikwa kwe nye Maandiko,“Tazama naweka jiwe huko Sayuni ambalo linawafanya watu kujikwaa na mwamba utakaowaangusha, na wale watakaomtegemea hawataaibika kamwe.”
Friday, 20 November 2015
UNAWEZAJE KUSHINDA DHAMBI?
Ninawezaje kushinda dhambi katika maisha yangu ya kikristo?
Swali: "Ninawezaje kushinda dhambi katika maisha yangu ya kikristo?"
Jibu: Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:
(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.
Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.
Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza 10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso 5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.
(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema. Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12 inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua. Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.
Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya nzuri kiroho.
Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu. Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya kiroho (Waefeso 6:12-18)!
(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi (Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15, na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!
Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo (Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa kwanza 5:14-15).
(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1). Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20). Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe, vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi (Mhubiri 4:11-12).
Baadhi ya watu ninaowafahamu wamepata kaka na dada katika kristo wanaotangamana pamoja au kwa simu na wanaelezana vile wanaendelea na maisha ndani ya kristo na wanawajibika katika kuombeana huku wakiishi maisha sawa na Neno la Mungu. Mabadiliko mara nyingine huja haraka na wakati mwengine polepole. Lakini Mungu ametuahidi ya kwamba kadri tunavyoendelea kutumia njia hizi alizotuwekea, ndivyo atatuletea mabadiliko maishani mwetu. Vumilia ukijua ya kuwa ni mwaminifu katika ahadi zake.
Subscribe to:
Posts (Atom)