Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa
maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema
mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya
uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima
| ||
Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16). Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni… A) Neno la Mungu li Hai B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6). C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11). b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11). c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6). Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12). Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo. Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11). Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35). Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3). |
Friday, 4 December 2015
UMUHIMU WA NENO LA MUNGU
UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Barikiwa sana MTU wa Mungu
ReplyDeleteasante kwa ujumbe
ReplyDelete