Friday 11 December 2015

YACHUNGUZE MAANDIKO

  NIWZEJE KUMPOKEA NA KUTOKA KATIKA MAUTI

1.Kiri mambo matatu

 A.Mimi ni mwenye dhambi."Wote wametenda dhambi " RUM 3:23

B.Niko hatarini kufa."Mshahara wa  dhambi no mauti"Rum 6:23

C.Siwezi kujiokoa ."Pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote"Yn 15:5

2.Baada ya toba hiyo amini   mambo matatu

A.Alikufa kwa ajili Yangu."Aionje mauti kwa ajili ya kila MTU" Ebr 2:9

B.Amenisamehe.
 C..Ameniokoa.

 YATAFAKARI MAMBO HAYA KWA MUDA 

#kwa sababu ya dhambi zangu nimehukumiwa kifo.

#siwezi kulipa fidia hiyo bila kupoteza uzima wa milele .

#ninadaiwa deni nisiloweza kulilipa.

#ni lazima niipokee zawadi hii.
















Friday 4 December 2015

UMUHIMU WA NENO LA MUNGU

UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU
Tokeo la picha la neno la munguUpo umuhimu wa kujua neno la Mungu katika maisha ya Mkristo halisi.
 
Biblia  inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
Kwa kusema hivyo kuna  umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima

Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16).
Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni…
A) Neno la Mungu li Hai
B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6).
C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga
D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake
E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo
KWA NINI NENO LA MUNGU LI HAI?
Neno la Mungu li hai kwa sababu  Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana
a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11).
b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11).
c) Neno la Mungu  li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“  Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu  pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6).
Uhai wa Neno la Mungu kwa mtu ndio unaoleta kushinda dhambi. Nao wakamshinda kwa neno la ushuhuda wao (Ufunuo 12:11).
Daudi aligundua au kwa maneno mengine alifahamu umuhimu wa neno la Mungu katika maisha, kama vile mtume Paulo anavyosema na Wakolosai kwa habari ya neno la Kristo kwamba likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu
Neno la Mungu lina nguvu na ndio maana  tunamshinda  shetani kwa neno la Mungu.
Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12).
Katika mistari hiyo tunaona Yesu anamwambia  shetani  ”imeandikwa“   Shetani nae anageuza usemi nae anamwambia Yesu ”imeandikwa kwamba atakuagizia malaika usije ukajikwaa mguu wako.“ Kwa kuwaYesu neno la Mungu limo ndani yake hamwambii tena shetani imeandikwa ila anamwambia imenenwa. Kwa maneno mengine tukiwa na neno la Yesu ndani yetu hatuwezi kuyumbishwa. Kwanini? Kwa sababu tumeshaona jinsi ambavyo shetani  anajaribu kutumia neno la Mungu   kwa kusema ”imeandikwa.“  Na ni kweli imeandikwa ananukuu kutoka kitabu cha Zaburi 91 :1-12. Hata kama shetani ananukuu maandiko haina sababu  yamimi kushindwa na shetani  maana Yesu tayari alikwisha mshinda. Yesu kumshinda shetani ina nipelekea mimi kusoma neno la Mungu kwa bidii sana. Kwa mfano, ni kweli kabisa imeandikwa mtakula vitu vya kufisha havitawadhuru lakini je, ninywe sumu sitakufa kwa sababu imeandikwa? Hapana, ukinywa hakika utakufa. Shetani hutumia mandiko kuwafunga wasiojua neno la KristoYesu.
Katika Biblia tunasoma pia kwamba ”imeandikwa“ Wanandoa MKE na MUME wasinyimane. Kwa kutojua neno vijana wa kiume na wa kike wamedanganywa. Si hao tu hata walioko kwenye ndoa wametegwa kwa andiko hilo. Neno linasema katika Mithali 6:32 ”Aziniye na mwanamke hana akili kabisa“ na Mwanamke vivyo hivyo akizini na mwanaume hana akili kabisa. Watu wamepata hasara ya mambo mengi kwa kutojua neno la Mungu. Ili tuweze kumshinda shetani  ni lazima  neno la Yesu liwe ndani  yetu ndiposa tutamshinda shetani. Ayubu kwa neno la Mungu alishinda. (Ayubu 19:25-27, Waefeso 6:17).
Nataka nikwambie neno la Mungu ni msaada katika maisha yetu maana hutupa  majibu ya maisha yetu. Katika Luka 5:3-6 tunasoma jinsi Petro na wenzake walivyopata samaki wengi kwa kutii neno la Kristo. Kumbuka pia juu ya yule akida, alimwambia Yesu ”...sema neno tu na mtumwa wangu atapona“ (Luka 7:2-10). Yesu akisema neno lazima mabadiliko yatokee.
Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga. Kwa nini neno la Mungu  lina ukali kuliko upanga? Upanga unaweza kukukata na usipone. Lakini neno linakata na kuponya. Kwa neno hili wafalme wanatubu. Yona alitumia neno la Mungu likawa kali watu wakatubu. (Yona 3:1-10; Matendo ya Mitume 8:18-24).
Neno la Mungu linachoma hata kuzigawa nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (Matendo 7:51-54, Yohana 4:16 -18, 27-29). Mwanamke akaambiwa mambo yake; Neno likachambua kila tabia..
Neno la Mungu li jepesi kutambua mawazo na makusudi ya moyo.
Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la  Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo.
Mtume Petro aliyependa kujua neno la Mungu, naye pia Mungu alimjalia neema ya kuyajua makusudi ya moyo wa mwanadamu (Matendo 5:1-11). Elisha aliyajua makusudi ya moyo wa mfalme ya kuwatenda Israeli kwa siri ila Mungu alimpa neema ya kuyajua mawazo ya mfalme (2 Wafalme 6:8-12).
Hili ni jambo la msingi katika maisha ya Mkristo yaani kulijua neno la Mungu. Neno la Mungu  tukiwa nalo na likitenda kazi ndani yetu lazima tufanikiwe (Yoshua 1:8) .
Je unahitaji kuwa na imani katika neno la Mungu? Basi, ni neno la Mungu peke yake ambalo laweza kuumba imani, maana pasipo neno la Mungu hakuna imani (Waebrania 11:3 ; Warumi10:17). Ili uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ulijue neno la Mungu na kulishika.(Yohana 8:31 ; Luka 2:19). Kama neno halimo ndani yetu tunayoyafanya yanakuwa hayana Mungu, hata twaweza kusalitiana. Mtu anayelitamani neno la Yesu  huling’ang’ania na kulitenda maana kwake ni nguvu. (1Wakorintho 1:18). Si kwamba Neno la Mungu ni nguvu tu: bali huleta faida (Mathayo 13:23).
Watu wengi tunapotea kwa kutokujua uwezo (nguvu) iliyomo katika neno la Mungu (Mathayo 22:29).
Yesu anasema, mtu anayelitenda neno la Mungu na kulishika huyo amepanda mbegu ambayo itazaa sana, maana ndani ya moyo wake imo mbegu ambayo ni neno la Mungu la uponyaji na mafanikio, msamaha, utu wema na mengi yanayofanana na hayo.
Yapaswa maisha yetu yawe yenye neno (mbegu) la  Mungu ili tuweze kuzaa mambo mazuri.
 

Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11).  Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35).
 
Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3).
 

Thursday 3 December 2015

MUNGU HANA UPENDELEO

Warumi 9:14-33

Mungu Hana Upendeleo

Tokeo la picha la GOD LOVES TO MAN14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.
19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?
22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa? 23 Na tunajuaje kama Mungu alifanya hivi ili kuwadhihirishia utajiri wa utukufu wake wale anaowahurumia, ambao aliwaandaa tangu mwanzo kupokea utu kufu? 24 Na sisi ndio hao walioitwa, si kutoka kwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko

25 Hivi ndivyo Mungu asemavyo katika kitabu cha Hosea, “Wale ambao hawakuwa watu wangu, nitawaita ‘watu wangu,’ na wale ambao hawakuwa wapendwa wangu, nitawaita ‘wapendwa wangu’.” 26 Na pale pale walipoambiwa,“Ninyi si ‘watu wangu,’ ndipo watakapoitwa, ‘Wana wa Mungu aliye hai’.” 27 Na Isaya anasema hivi kuhusu Israeli: “Ijapokuwa wana wa Israeli watakuwa wengi kama mchanga wa bahari, ni wachache tu miongoni mwao watakaooko lewa;
28 kwa maana Mungu ataitekeleza hukumu yakejuu ya ulimwengu mara moja na kuikamilisha.” 29 Na tena kama alivyotabiri Isaya,“Kama Bwana wa majeshi asingetuachia uzao, tungalikuwa kama Sodoma, na kufanywa kama Gomora.”
30 Kwa hiyo tusemeje basi? Watu wa mataifa ambao hawakuta futa kupata haki wamepewa haki kwa njia ya imani. 31 Lakini Waisraeli ambao wametafuta kupata haki kwa msingi wa sheria, hawakuipata kwa maana hawakutimiza sheria. 32 Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani bali kwa kutegemea matendo. Wali jikwaa kwenye lile ‘jiwe la kujikwaa.’ 33 Kama ilivyoandikwa kwe nye Maandiko,“Tazama naweka jiwe huko Sayuni ambalo linawafanya watu kujikwaa na mwamba utakaowaangusha, na wale watakaomtegemea hawataaibika kamwe.”