Kwa nini kuna mivutano ya siku za Ibada ?
Tangu mwanzo, Biblia inasemaje juu ya suala la kumwabudu Mungu ?
1. 1. Je, Mungu aliwaagiza watu waitunze Sabato ?
Jibu : Ndiyo ! Ushahidi wa Biblia.
Mwanzo 2:2-3… “Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote
aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote
aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu
katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote
aliyoiumba na kuifanya”.
1. 2. Je, Adamu na Ibrahimu waliitunza Sabato?
Jibu : Ndiyo ! Ushahidi wa Biblia
Mwanzo 2:2-3. Adamu aliitunza Sabato
Mwanzo 26:5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi
maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
Ibrahimu alitunza Amri za Mungu ikiwemo na Sabato(Amri ya Nne).
1. 3. Je, kuna Amri yoyote inatutaka tuitunze Sabato?
Jibu : Ndiyo ! Ushahidi wa Biblia.
Kutoka 20:8-11 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi,
utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu
wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti
yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga,
wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana
alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku
ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
(linganisha na Mwanzo 2:2-3)
4. Siku ya Sabato ni ipi ndani ya Juma?
Jibu: Jumamosi! Ushahidi wa Biblia.
Ndani ya Biblia hakuna majina ya siku ya Jumatatu, Jumanne, n.k.
isipokuwa kwa Biblia ya Kiswahili cha Kisasa. Ndani ya Biblia Mungu
aliziita siku ya kwanza, pili, tatu, n.k (Mwanzo 1…).
Kibiblia Yesu alifufuka siku ya Kwanza ya Juma, yaani Jumapili. Fanya
hesabu rahisi! Siku ya Saba itakuwa ni lini? Daima ni Jumamosi.
Majina haya yalitokea wapi?
Mf: Kiingereza
1. Sunday , siku ya jua, siku ya mungu mume wa Roma ya kale ya kipagani.
2. Monday, siku ya mwezi, mungu mke wa Roma ya kale ya kipagani.
3. Tuesday, siku ya mungu tuis wa Roma ya kale ya kipagani.
4. Wednesday, siku ya mungu wenes wa Roma ya kale ya kipagani.
5. Thursday, siku ya mungu thrus wa Roma ya kale ya kipagani.
6. Friday, siku ya mungu frigus wa Roma ya kale ya kipagani.
7. Saturday, siku ya mungu satun wa Roma ya kale ya kipagani.
Kiswahili:
Waswahili wao walifuata utaratibu wa waarabu katika kuita siku majina.
Lengo la waarabu, ni kuifanya siku ya ijumaa kuwa siku ya saba(siku ya
kusanyiko la ibaada). Lakini pamoja na jitihada zao hizo, walichemka
mahali. Fuatilia uone!!
1. Jumamosi, siku ya kwanza ya juma
2. Jumapili, siku ya pili ya juma
3. Jumatatu, siku ya tatu ya juma
4. Jumanne, siku ya nne ya juma
5. Jumatano, siku ya tano ya juma
6. Alhamisi, (neno la kiarabu lenye maana ya –a tano=alhamsa) ya sita ya juma
7. Ijumaa, siku ya saba ya juma(sabato ya waarabu/waislamu)
Jiulize, utatokaje ya tano(Jumatano) uende ya tano(alhamisi) tena??
Msaada zaidi, angalia kamusi zozote za Kiingereza za zamani,
zitakupatia maana halisi za majina ya siku. Mf. Collins English
Dictionary, 1979 reprited on 1984.
Uthibitisho wa kibiblia unaonesha kuwa, siku ya Sabato ni Jumamosi kama leo inavyojulikana. Angalia!
Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya
juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama
kaburi.
Marko 16:2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea
kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.
Luka 24:1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda
kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa
kaburini.
Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo
wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama
katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Yesu alifufuka siku ya jumapili ambayo Biblia inaiita kuwa ni siku ya
kwanza ya juma. Kama Yesu alifufufuka siku ya kwanza ya juma(jumapili),
Sabato itakuwa lini??
Jibu: Jumamosi
1. 5. Je, Yesu alifundisha kuishika Sabato??
Jibu: Ndiyo! Yesu ni kielelzo chetu kwa matendo yake na mwenendo wake wa
maisha. Chochote alichokifanya na kukisema Yesu, ni sharti tukienzi…
Marko 1:21 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
Marko 6:2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi
waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni
hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa
inayotendeka kwa mikono yake?
Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia
katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Luka 4:31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;
Luka 13:10 Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.
Luka 6:6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi
akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.
1. 6. Je, kanisa la awali lilikutana siku ya Sabato kuabudu?
Jibu: Ndiyo. Mitume wa Yesu na mitume waliofuata walikutana siku ya sabato kuabudu.
Ushahidi wa Biblia:
Matendo ya Mitume 13:14 Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya
nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku
ya sabato, wakaketi.
Matendo ya Mitume 13:27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa
kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato,
wameyatimiza kwa kumhukumu.
Matendo ya Mitume 13:42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.
Matendo ya Mitume 13:44 Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.
Matendo ya Mitume 15:21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu
wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika
masinagogi.
Matendo ya Mitume 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango,
tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali;
tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Matendo ya Mitume 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia
mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
Matendo ya Mitume 18:4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani
Paulo bado anasisitiza
Waebrania 4:9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
7.Je, Mungu ana watu wake maalumu tu?
Jibu :Ndiyo
Math 7 :21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika
ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni.
Je, mapenzi ya Baba yake ni yapi ?
Zaburi 40 :8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
1. 8. Je, mtu anaweza kumpenda Yesu bila kushika Amri zake 10?
Hasha!! Yeye anasema;
Yoh 14:15(mkinipenda mtazishika amri zangu)
Yohana 14:21 (Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye
anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na
kujidhihirisha kwake).
Yohana 15:10 (Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama
vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake).
1. 9. Je, inawezekana kushika Amri 9 tu isipokuwa Sabato?
Hasha!! Haiwezekani kabisa, Biblia inasema;
Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
1 Yohna 2:3-5 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa
tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake,
ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno
lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili
twajua ya kuwa tumo ndani yake.
1 Yohana 5:2-3 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu,
tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda
Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
1. 10. Je, Sabato itakuwepo hadi mbinguni ?
Jibu : Ndiyo
Nabii Isaya alioneshwa watakatifu wakienda mbele za Mungu kuabudu siku
ya Sabato mbinguni. Yohana naye alioneshwa sanduku la Agano (la Amri 10
ikiwemo sabato) liko hekalu la mbinguni.
Isaya 66 :22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya,
zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu
litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata
sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Ufunuo 11 : 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa,
na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na
umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi
sana.
1. 11. Je kuna haja ya kutunza Sabato leo?
Jibu : Ndiyo. Kuitunza Sabato ya siku ya saba (Jumamosi) ni kumtangaza
Mungu kuwa ni Mkuu, Muumbaji na Mwenye Vyote ! Shetani anajitahidi sana
kufumba uelewa wa watu wasilitambue hili na kuendelea kumwadubu yeye
mungu wa dunia hii. Tunaposali Jumapili au Ijumaa, tunamkana Mungu kuwa
si Muumbaji, Mkuu na Mwenye vyote. Rejea Amri ya 4 Kutoka 20 :8-11
Hakuna wokovu kwa waliokwisha sikia habari za Sabato ya Yahwe watakaokolewa .
Mpinga Kristo ameibuka na kuleta mafundisho potofu na kinyume cha
makusudi ya Mungu. Anatumia manabii, wachungaji, walimu nk kufundisha
watu mapotofu, wakidai Bwana Mungu alisema hivi ijapo Bwana Mungu
hakusema lolote…
Ezekieli 22:26Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi
vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu
vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu
vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie
sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.
Wapendwa kuna haja ya kuchunguza hili kwa makini, tuache ubishi wa
kidini badala yake, tuangalie sana kuyatenda mapenzi ya Mungu ambayo ni
kushika Amri zake.
Zaburi 40:8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyofuraha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Sheria ya Mungu inapokaa mioyoni mwetu, tutazishika Amri zake zote 10
kama vigezo vya sisi kwenda mbinguni. Tusipoenenda sawasawa na neno
lake, hakuna asubuhi kwetu…
‘Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi’. Isaya 8 :20.
Chagueni hivi ni nani mtakayemtumikia kuwa ni Mungu au Baali(Shetani
na sabato yake bandia). Mimi nitamtumikia Mungu(Yahwe) na Sabato yake
halisi(Muhuri wake).
Hatari ya kutomtii Mungu
Ezekiel 20:21 Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu,
wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi
kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi sabato zangu, ndipo nikasema,
kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu
yao jangwani.
Wito wa Mungu kwetu
Ezekiel 20 :19 Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;
20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu