Tuesday 12 July 2016

SODA NINI KATIKA MWILI WAKO?

Image result for soda
Inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka. japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku amabayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.

1. Ugonjwa wa kisukari; kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya ili insulini nyingi kushusha sukari. muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.

 2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.

3. Upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.

4. Ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.

5. Huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.

6. Hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kua na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.

7. Addiction; soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.

8. Huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.

9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice ya matunda yakutengeneza mwenyewe ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.

Tuesday 5 July 2016

UNAKARIBISHWA

JE , WEWE UNATAMBUA ?



Uimbaji ni moja ya kalama ambayo Mungu alimpatia mwanadamu ili amsifu .Mungu anasema mnitukuze kwa nyimbo , matendo mema na hiyo ndio ibada kamili kwangu.







wahubiri wengi wanafanya kazi pamoja na waimbaji katika ulimwengu
huu , wanadamu wote haijarishi unakalama au hauna lazima ufanye
kwa nafasi yako , kama kuhubiri hubiri kama kuimba imba ,kama
kufundisha fundisha ,kama kushuhudia shuhudia kwa kufanya hivyo
kristo anatukuzwa.

Monday 4 July 2016

WEWE UKARIBU YA NANI?

NENO LA LEO - MTAZAME ALIYE KARIBU NAWE

 Zaburi:34:18 "Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa".

Ni jambo la kawaida kuona watu wakihangaika kutafuta msaada juu ya changamoto zinazo wapata. Ndivyo tunashuhudia wengine wanachukua maamuzi magumu hata ya kujiua, baada ya kushindwa kupata msaada. Hebu kila mmoja apige picha, tatizo linapotokea, nani anakuwa wa kwanza kumwendea ili kupata msaada? Wengi watakuambia, ni wazazi, au mume, au mke, au Rafiki, au daktari bingwa, au Mchungaji n.k. kutokana na aina ya tatizo.

Neno la leo linatukumbusha kuwa; mbali na kumtegemea mtu fulani mwenye uwezo wa kukusaidia unapopitia machungu katika maisha haya, Karibu yako yupo Mungu mwenye uwezo zaidi ya wote wanaoweza kutegemewa. Mara nyingi shetani ametudanganya na kututenga na Upendo wa Mungu, na hatimaye akitujeruhi, tunakosa ujasiri wa kuutegemea mkono wa Mungu, macho huwa hayaoni, giza la machungu na simanzi huujaza moyo, na hatimaye wengine, huamua kujiua, wengine huishia kuugua vidonda vya tumbo na shinikizo la damu.

Kumbuka, mwanadamu yeyote sio wa kutegemewa, wakati wowote anaweza kugeuka au hali ikabadilika, wengi wamejeruhiwa na wenzi wao waliokuwa wameijaza mioyo yao, na wameishia kuathirika kwa namna fulani, katika hali kama hiyo ni Mungu pekee aliye Karibu sana na kila mmoja, anaweza kukuokoa katika hali ya kuvunjika moyo.

Unapojeruhiwa na kuumizwa moyo, iwe kwa magonjwa, iwe kwa kuteswa na nguvu za uchawi au majini, iwe kwa kukosa ajira, iwe kwa kushindwa masomo, iwe kwa umaskini, iwe kwa kufiwa na mwenzi, iwe kwa biashara kuporomoka, iwe kuonewa kazini, iwe kwa kukosa mchumba, iwe kwa mwenzi wa ndoa kukutesa kimahusiano, iwe ni kutengwa na marafiki, iwe ni kuonewa na ndugu, iwe ni changamoto yoyote inayo kuumiza na kujeruhi moyo wako; Mungu yuko Karibu nawe KUKUOKOA, mtazame yeye utakuwa salama. Yesu alikufa kwa ajili yetu, ili tuokolewe na kupatanishwa na Mungu Baba, mtazame yeye Uokolewe.